July 10, 2016


Nahodha wa Yanga, Nadir Haroub ‘Cannavaro’ amesema wanataka kushinda kwa juhudi zote mechi dhidi ya Medeama siku chache zijazo.

Cannavaro amesema wamekuwa wakifanya mazoezi kwa juhudi kubwa, pia wanasikiliza kila ambacho makocha wao wanachowaelekeza, kwa kuwa wamelenga kufanya vizuri na si zaidi.

“Tunataka kufanya vizuri, kila mchezaji anataka kushinda. Usidhani wachezaji wanafurahia hali ya kupoteza.

“Hivyo tunaendelea na mazoezi kwa juhudi zote. Tunataka kushinda dhidi ya Medeama ili kufufua matumaini.”

Yanga imekuwa ikiendelea na mazoezi chini ya Kocha Hans va der Pluijm na wasaidizi wake Juma Mwambusi na Juma Pondamali.

Wachezaji Yanga wamekuwa wakifanya mazoezi ya nguvu pamoja na kucheza utafikiri wako kwenye mechi hali inayothibitisha kweli hawana mchezo na wamepania kushinda.


Yanga inatakiwa kushinda mechi dhidi ya Medeama ili kuibua matumaini. Maana tayari imepoteza mechi mbili hivyo kama haitashinda, itakuwa imemaliza matumaini ya kuendelea kupambana kucheza nusu fainali ya Kombe la Shirikisho ikitokea Kundi A

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV