July 31, 2016


Mfanyabiashara Mohammed Dewji maarufu kama Mo, ametawala katika mkutano wa wanachama wa Simaba uliofanyika leo jijini Dar es Salaam.

Wanachama walionekana wazi kuwa wana hamu ya kuusikia uongozi wao unasema nini kuhusiana na kuingia kwenye kampuni ambako Simba itaweza kuuza hisa.

Uamuzi huo, ulisababisha wanachama kutotaka kujadili chochote zaidi ya kuona kama uongozi uko tayari kuuza hisa zake asilimia 51 kwa Sh bilioni 20 kwa Mo.

Wakati wa kujadili ajenda nyingine za kikao kama zile za Hesabu, Chombo cha uchaguzi na kadhalika, hazikuwa na mvuto na wengi walitaka ajenda namba tisa ambayo ilikuwa ni “Taarifa ya kamati ya maboresho ya mfumo wa uendeshaji”.

Lakini wanachama hao walianza kulalamika wakiona kama uongozi ulipita haraka hapo. Wakaanza kupiga kelele wakitaka kusikia mjadala.

Mwisho, Rais wa Simba Evans Avena alilazimika kurejea na kuwaeleza kwamba kama wanataka Simba kuingia kwenye mchakato wa kampuni, maoni yao yamesikilizwa na yanaanza kufanyiwa kazi.

Kauli hiyo ya Aveva, ilifanya wanachama hao washangilie kwa nguvu hata yeye baada ya kuufunga mkutano huo.



0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic