Uwanja wa Simba uliopo Bunju umeanza kukwanguliwa lakini imeelezwa kutamwagwa kifusi zaidi ya tani 100 tena.
Imeelezwa baad ya zoezi hilo, kitakachofuata ni suala la kusawazisha kabla ya kuanza kuwekwa kwa nyasi bandia.
Hivyo pamoja na zoezi la kuukwangua uwanja, inaonekana ndiyo mwanzo kabisa na zoezi bado.
Uongozi wa Simba umeanza kulifanyia kazi zoezi hilo takribani wiki sasa na mambo yamekuwa yakienda kimyakimya.
Taarifa za ndani zinaeleza, uwanja utakuwa ni kwa ajili ya mazoezi na baada ya hapo zitajengwa hosteli kwa ajili ya wachezaji kuweka kambi.
Halafu baada ya hapo kutakuwa na mwendelezo wa kuanza kujengwa majukwaa ya muda na mabadiliko yatafuatia kuwa majukwaa ya kudumu kulingana na uongozi ulio madarakani unatakaje.
0 COMMENTS:
Post a Comment