February 8, 2017Meneja wa Simba, Mussa Hassan Mgosi amesema wanajua mechi yao dhidi ya Prisons ni Jumamosi na maandalizi yanakwenda vizuri.

Katika mechi ya mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu Bara, Simba ililala kwa kuchapwa mabao 2-1 dhidi ya Prisons mjini Mbeya na sasa inachotaka ni kulipa kisasi.

Mgosi amesema kumekuwa na taarifa kwamba huenda mechi hiyo imeahirishwa, jambo ambalo hawalijui.

“Sisi tunaendelea na maandalizi kwa ajili ya mechi yetu Jumamosi, sasa kama kuna mtu anasema imeahirishwa sisi hatuna taarifa hiyo,” alisema Mgosi akionekana kujiamini.

Simba inashika nafasi ya pili kwa tofauti ya pointi moja dhidi ya mabingwa watetezi, Yanga walio kileleni.


Mechi yake ya mwisho, Simba iliitwanga Majimaji kwao Songea kwa mabao 3-0 katika mechi ambayo ilionyesha kiwango na kurejesha matumaini.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV