October 4, 2017




Kiungo huyo kutumia viatu hivyo katika mechi za uwanja huo kutokana na hali ya uwanja wenyewe ambao ni mgumu  na haufai kwa wachezaji wenye majeraha.

“Mechi dhidi ya Mtibwa, Kamusoko hakutumia viatu aina ya njumu vile meno makubwa chini na badala yake alilaizimika kutumia viatu vyenye meno madogo ‘training shoes’ kutokana na ubovu wa uwanja wa Uhuru ambao ni mgumu unaoweza kumsababisha mchezaji aliyetoka kwenye majeraha kama Kamusoko kuumia tena.

“Kama unakumbuka siku mbili kabla ya mechi na Mtibwa, Kamusoko alishindwa kuendelea na mazoezi kwenye uwanja huo, hiyo ni baada ya kujitonyesha goti, hivyo daktari akashauri atumie viatu spesho atakavyovitumia katika mechi watakazozicheza katika uwanja huo,”alisema mtoa taarifa huyo.

Alipotafutwa Bavu kuzungumzia hilo alisema kuwa “Kiukweli Uwanja wa Uhuru ni mbaya, sehemu ya ‘pitch’ ni ngumu ambayo nina hofu ya kuongezeka kwa majeruhi kwenye timu.


“Mechi na Mtibwa ni kweli Kamusoko alivaa viatu vyenye meno madogo ambavyo ni maalum kwa viwanja vyenye ‘pitch’ ngumu kama ilivyokuwa ya Uhuru, hivyo nikamshauri atumie viatu hivyo kwa hofu ya kujitonyesha,”alisema Bavu.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic