October 4, 2017



Baba mzazi wa kipa wa Singida United, Peter Manyika, Manyika Peter, ameibuka na kutaja  vitu vilivyosababisha kushuka kwa kiwango cha mtoto wake akiwa Simba na kusema sababu kubwa ni ujana ulimsumbua.


Manyika alijiunga na Simba misimu miwili iliyopita lakini hakuweza kufanya vizuri kutokana na kukosa namba ya kudumu kwenye timu hiyo kabla ya kujiunga na Singida United pamoja na  kipa wa zamani wa Yanga, Ally Mustafa ‘Barthez’.

Barthez mpaka sasa hajacheza mechi yoyote ligi tangu ianze mbele ya Manyika aliyedaka mechi zote tano akiruhusu mabao manne huku wakifanikiwa kupata pointi kumi.

 Peter ambaye ni kipa wa zamani wa Yanga na Taifa Stars, alisema kubadilika kwa kipa huyo kumetokana na kutambua thamani yake baada ya kuacha mambo ya kitoto na ujana wakati akiwa Simba.


“Unajua yeye mwenyewe alijichanganya na kuna wakati alishuka kiwango kabisa kutokana na matatizo yake mwenyewe ya ujana na adhabu alizozipata kama vile tulimfukuza kwenye kituo [cha kufundisha makipa kinachomilikiwa na Manyika", akawa hana sehemu ya kupata mazoezi makali, baadaye alishtuka ikabidi aombe msamaha kwenye kituo tukampokea lakini tulimpa masharti ndiyo maana sasa hivi unaona amebadilika sana,” alisema mzazi huyo.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic