October 23, 2017



Rekodi ya Kocha wa Simba, Mcameroon, Joseph Omog mbele ya Yanga, inamfanya kocha huyo kuingia uwanjani Jumamosi ijayo akiwa anajiamini kuliko mpinzani wake, George Lwandamina raia wa Zambia.

Jumamosi ijayo, Yanga itakuwa mwenyeji wa Simba kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara utakaopigwa katika Uwanja wa Uhuru jijini Dar.

Omog ambaye huu ni msimu wake wa pili ndani ya Simba, mpaka sasa amekutana na Yanga mara nne ambapo hajapoteza hata mechi moja baada ya kushinda tatu na sare moja.
Mechi ambazo Omog ameshinda dhidi ya Yanga ni ya Ligi Kuu Bara msimu uliopita Simba ilipoibuka na ushindi wa mabao 2-0. Omog akaiongoza tena Simba kuifunga Yanga kwa penalti 4-2 kwenye Kombe la Mapinduzi, kabla ya kuibuka tena na ushindi wa penalti 5-4 kwenye Ngao ya Jamii msimu huu.

Mechi ya sare ni ile ya ligi kuu msimu uliopita iliyomalizika kwa 1-1, wakati huo Yanga ilikuwa ikinolewa na Mholanzi, Hans van Der Pluijm ambaye kwa sasa yupo Singida United.
"Mechi baina ya Yanga huwa ni ngumu kutokana na upinzani uliopo baina ya timu hizi, lakini tutajipanga kupambana nao kuhakikisha tunaibuka na ushindi kuendeleza rekodi nzuri tuliyo nayo siku za hivi karibuni," alisema Omog.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic