October 23, 2017




Mkabaji katika kiungo cha Simba, Jonas Mkude ambaye awali katika mechi za kwanza za timu hiyo alikuwa akianzia benchi kutokana na kutokuwa na nafasi kwenye kikosi cha kwanza cha timu hiyo, amesema kuwa hivi sasa yupo vizuri na tayari kwa mapambano dhidi ya Yanga.

Mwanzoni mwa msimu huu Mkude alipoteza nafasi ya kucheza katika kikosi cha kwanza cha timu hiyo kutokana na ushindani wa namba kutoka kwa Mghana, James Kotei lakini hivi karibuni alirejea kwenye nafasi yake hiyo na mechi yake ya kwanza kuanza na kufanikiwa kucheza dakika zote 90 ilikuwa dhidi ya Mtibwa Sugar lakini pia akifanya hivyo juzi Jumamosi dhidi ya Njombe Mji.

Mkude alisema kuwa hivi sasa yupo vizuri na amejipanga kufanya makubwa katika mchezo dhidi ya Yanga kwa kukabiliana na kiungo wa timu hiyo raia wa DR Congo, Papy Tshishimbi.

Tshishimbi, hivi sasa ndiye nguzo kubwa ya Yanga katika safu ya kiungo kutokana na uwezo wake mkubwa wa kukaba na kuanzisha mashambulizi.

“Nashukuru Mungu kwa kunijalia afya njema lakini pia roho ya kutokata tamaa, baada ya mechi hii dhidi ya Njombe Mji sasa najiandaa kwa ajili ya Yanga.

“Najua mechi itakuwa ngumu lakini kwa jinsi nilivyo sasa najua hakuna wa kunisumbua katika nafasi ya kiungo, nitapambana na kila nitakayekutana naye endapo kocha wangu atanipatia nafasi ya kucheza.

“Sitaogopa mtu yeyote kama ilivyo kawaida yangu, hata kama ni Tshishimbi nitakula naye sahani moja,” alisema Mkude ambaye kwa sasa ndiye mchezaji mzawa ghali zaidi katika kikosi cha Simba.

SOURCE: CHAMPIONI


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic