February 4, 2018




FULL TIME
Mwamuzi anamaliza mchezo, Simba imepata ushindi wa mabao 3-0.
Dk ya 90+3: Adam Ibrahim wa Ruvu anapewa kadi ya pili ya njano.
Dk ya 90+2: Kasi ya mchezo imepungua.
Dk ya 90: Zinaongezwa dakika tatu za nyongeza.
Dk ya 86: Simba wanatengeneza mashambilizi lakini mipango inakwama.
Dk ya 84: Gyan anapiga shuti linalopanguliwa na kipa na kutoka nje ya lango, inakuwa kona.
Dk ya 82: Ruvu hawaonyeshi kukata tamaa.
Dk ya 79: Mwamuzi anampa kadi ya njano Erasto Nyoni wa Simba kutokana na kuchelewesha mpira.
Sk ya 78: Anatoka John Bocco anaingia Nicholaus Gyan.Dk ya 76: Mussa anashindwa kutumia vizuri pasi aliyopata.
John Bocco anaipatia Simba bao la tatu. Aliu-'chop' mpira nje ya eneo la 18 baada ya kipa kuwa ametokea kuudaka mpira.
Dk ya 74: GOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOO Dk ya 71: Mlipili wa Simba anapata kadi ya njano kwa mchezo mbaya.
Dk ya 71: Simba wanaoata faulo karibu na lango la Ruvu, inapigwa inaokolewa.
Dk ya 68: Simba wanapata bao la pili, mfungaji ni Mzamiru, anamalizia krosi ya Kichuya.
GOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOO
Dk ya 58: Ruvu wamewapunguza kasi Simba.
Dk ya 55: Bocco ametolewa nje anapatiwa matibabu.
Dk ya 54: Bocco yupo chini anatibiwa, ameumia goti wakti wa purukushani za kuwania mpira.
Dk ya 50: Mwinyi Kazimoto anapiga shuti linatoka nje kidogo la lango.Dk ya 47: Simba wanapata kona, inapigwa kipa anaokoa. Kipindi cha pili kimeanza.

Mabadiliko, Kazimoto kaingia, Said Ndemla wa Simba ametoka.
Timu zinaingia uwanjani.

MAPUMZIKO
Dk ya 45+3: Laudit Mavugo anaingia, Okwi anashindwa kuendelea na mchezo.
Dk ya 45+2: Mau Bofu anapewa kadi nyekundu.
Dk ya 45: Mchezo umesimama, Okwi anatibiwa, zinaongezwa dakika 3.

dK YA 45: Mau Bofu wa Ruvu anampiga makusudi Okwi usoni akiwa hana mpira.
Dk ya 43: Ndemla anapiga shuti almanusura liingie wavuni.
Dk ya 41: Kwasi anamtoka beki wa Ruvu, inapigwa krosi, inaokolewa.
Dk ya 37: Ruvu wanapata faulo nje kidogo ya eneo la lango la Simba, wanapiga inatoka nje. Dk ya 31: Issa Kanduru anapewa kadi ya njano kwa kumchezea faulo Shomari Kapombe.
Dk ya 29: Simba wanapata kona. Kichuya anapiga lakini inakosa mmaliziaji.
Dk ya 27: Simba wanafanya mashambulizi mara mbili ndani ya muda mfupi.
Dk ya 24: Mchezo unaendelea.
Dk ya 23: Wachezaji wa timu zote wanapumzika kidogo, jua ni kali, mwamuzi anawaruhusu wapumzike kwa dakika 1.
John Bocco anaipatia Simba bao kwa njia ya kichwa, aliunganisha mpira wa kona wa Shiza Kichuya.

GOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOO
Dk ya 21: Simba wanapata kona.
Dk ya 20: Simba wanafanya mashambulizi mfululizo.
Dk ya 18: Mau Bofu anapata kadi ya njano kwa kumchezea vibaya Okwi, alimpandishia mguu.
Dk ya 8: Adam wa Ruvu anapata kadi ya njano kwa kumzonga mwamuzi akilalamika.
Dk ya 5: Okwi tena anafika langoni mwa Ruvu lakini walinzi wa Ruvu wanakuwa makini kuokoa.
Dk ya 3: Simba wanafika langoni mwa Ruvu lakini Okwi anakosa umakini.

Dk ya 1: Kasi ya mchezo haijawa kubwa.
Mchezo umeanza.
Timu zinaingia uwanjani.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic