KOCHA MBEYA CITY: SIMBA NA YANGA SI TIMU KUBWA, NI ZA KAWAIDA MNO
Kocha wa klabu ya Mbeya City, Ramadhan Nswanzurwimo, haoni ukubwa wa timu za Yanga na Simba kwa kueleza kuwa havina utofauti wowote timu yake.
Nswazurwimo ametamka maneno hayo baada ya kichapo cha mabao matatu kwa moja dhidi ya Simba katika mchezo wa Ligi Kuu Bara uliopigwa jana kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa Sports Xtra, Kocha huyo alisema kuwa Yanga na Simba si timu kubwa huku akieleza kuwa zote pamoja na Mbeya City ziko kwenye levo moja.
Mbali na hilo, Nswazurwino alisema utofauti wa Mbeya City na timu hizo upo katika ligi tu ambapo timu moja inafanya vizuri huku nyingine ikiwa haifanyi vizuri.
"Yanga na Simba si timu kubwa, utofauti unakuja kwenye eneo moja pekee ambapo timu moja inafanya vizuri kwenye ligi huku nyingine ikiwa haifanyi vizuri, timu zote ziko kwenye levo moja hivyo Yanga na Simba zi timu kubwa" alisema.








Hivyo idadi ya wanachama na mashabiki wa Mbeya city na Simba au Yanga upo sawa? Huyu Kocha anajua maana ya ukubwa wa Timu au anaropkwa tu?
ReplyDeleteSasa kama huyu kocha angeshinda hii machi maneno yake yangekuaje?
Hahahahahahahahaaaa...kwahyo Tanzania hakuna timu kubwa? Kuna wakati dharau km hizi zinawaponza baadhi ya makocha
ReplyDelete