April 13, 2018



Nahodha wa kikosi cha Azam FC, Himid Mao, anaamini mvua ya jana imetia baraka zaidi kuelekea mchezo wa leo katika ligi dhidi ya Ruvu Shooting FC.

Kunyesha kwa mvua jana kulisababisha mechi hiyo kuahirishwa baada ya Uwanja wa Mabatini kujaa maji hivyo itabidi ucheze leo saa 10 jioni.

Mao alisema kutofanyika kwa mchezo huo siku ya jana kumewapa nafasi ya kupumzika na kuwaweka fiti zaidi kucheza leo.

"Mimi naona kama imekuwa jambo jema kwani tumepata mwanya wa kupumzika na kutuweka fiti zaidi, ukiangalia tumetoka kucheza mechi na Mbeya City siku kadhaa zilizopita" alisema Mao.

Kikosi cha Azam kitakuwa ugenini Mabatini Stadium mjini Mlandizi jioni ya leo kukipiga na Ruvu Shooting.

Ushindi wa Azam utaifanya ipande mpaka nafasi ya pili kwa kufikisha alama 48 kwenye msimamo wa Ligi na kuishusha Yanga ambayo ina alama 47 kwenye nafasi ya tatu. 


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic