April 4, 2018



Baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 ikiwa ugenini dhidi ya Njombe Mji FC jana, uongozi Simba wasema ulipata matokeo katika Uwanja ambao si rafiki.

Kupitia Afisa Habari wa timu hiyo, Haji Manara, alisema Uwanja wa Sabasaba haukuwa na hadhi ya kuchezea mechi kutokana na pichi yake kutoridhishwa.

Mbali na kutoridhishwa na Uwanja, Manara alieleza kuwa kwa sasa wanaanza kujiandaa na mchezo mwingine dhidi ya Mtibwa Sugar huku wakiweka pembeni yaliyojiri mjini Njombe.

"Tumepata matokeo katika uwanja ambao haukuwa rafiki kwetu, hilo limeshapita na sasa tunajipanga kwa mchezo unaokuja dhidi ya Mtibwa" alisema Manara.

Simba ilifanikiwa kupata mabao yake jana kupitia John Bocco aliyefungwa katika dakika za 14 na 64.

Simba sasa itakuwa inaanza maandalizi ya mchezo mwingine wa ligi kuanzia kesho dhidi ya Mtibwa Sugar, utakaopigwa Jamhuri Stadium, mwishoni mwa wiki hii.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic