April 4, 2018



Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa klabu ya Simba, Haji Manara, amesema walichojifunza kuhusiana na matokeo ya mchezo dhidi ya Njombe Mji FC jana.

Akizungumza mapema baada ya mchezo huo kumalizika, Manara alieleza wameona changamoto ya Uwanja namna ilivyokuwa kutokana na pichi yake kushindwa kuhimili mikiki ya mchezo kwa ujumla.

Aidha Manara anaamini benchi la ufundi lina uzoefu na mechi za ugenini, hivyo analiachia kufanya kazi yake kujipanga na michezo ijayo.

Manara alisema benchi la ufundi chini ya Kocha Pierre Lechantre, litatumia maarifa yake vizuri kujiandaa na michezo ijayo dhidi ya Mtibwa Sugar na Tanzania Prisons inayokuja mbele.

Matokeo hayo ya jana yaliifanya Simba iendelee kujikita kileleni kwa kufikisha jumla ya alama 49, nyuma ya watani wao wa jadi Yanga walio na 46.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic