April 27, 2018



Taasisi ya Lengo Football Academy yenye makazi yake Mkoani Arusha nchini Tanzania na Australia imeteua vijana wawili wa Tanzania wenye umri wa miaka 12 Laigwanani Lomayani Mollel na Ziporah Mollel katika mpango wake unaofahamika kama  Football For Friendship.
Mpango huo wa Football For Friendship(F4F2018) umelenga katika vijana wadogo kuwa promoti,kuwakuza na kuwajenga katika kuupenda mpira.
Mpango huo wa F4F2018 umelenga kwenye kupata mchezaji mmoja na mwandishi mmoja wote wakiwa ni vijana wenye umri wa miaka 12.
Laigwanani ambaye ni mchezaji na Ziporah ambaye ni Mwandishi watapelekwa nchini Russia wakati wa Fainali za Kombe la dunia zitakazofanyika mwaka huu nchini humo wakiambatana na watu wazima wawili watakaokuwa wakiwaangalia.

Wakiwa Russia watapata nafasi ya kucheza mechi mbalimbali na wenzao kutoka nchi tofauti huku pia wakipata nafasi ya kushuhudia mechi kadhaa za kombe la dunia.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic