Kocha mkongwe nchini, Abdallah ‘King Mputa’
Kibadeni amesema yuko tayari kuanza kufanya kazi Simba na kikubwa kwake ni
maslahi.
Kibadeni amesema hata kama Kagera Sugar ambao
mkataba wake naye umeisha watampa maslahi mazuri zaidi, basi atendelea kufanya
nao kazi.
“Mimi ni kocha, hii ndiyo kazi yangu. Kikubwa hapa
ninaangalia maslahi, kama Kagera watakuwa wamenipa mazuri zaidi nitabaki.
“Lakini kama watashindwa basi niko tayari kuondoka
na kuangalia timu nyingine,” alisema na alipoulizwa kama yuko tayari kuanza
kazi Simba ambayo amefanya nayo mazungumzo, alisema.
“Ndiyo, niko tayari kama tutakuwa tumekubaliana na
suala la maslahi yangu limetekelezwa.”
Taarifa za uhakika zinaeleza, Simba iko katika
hatua za mwisho za kumalizana na Kibadeni na anatarajia kuanza kazi mwanzoni
mwa mwezi ujao kukinoa kikosi hicho kwa ajili ya michuano ya Kombe la Kagame na
maandalizi ya Ligi Kuu Bara msimu ujao.
0 COMMENTS:
Post a Comment