April 2, 2018



Kikosi cha Welayta Dicha kinatarajia kuwasili nchini wiki hii kutokea Ethiopia kwa ajili ya mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Yanga.

Waethiopia hao watakuwa na kibarua Jumamosi ya wiki hii Aprili 7 2018 katika Uwanja wa Taifa kuanzia majira ya saa 10 kamili jioni.

Welayta wako nafasi ya 8 kwenye msimamo wa ligi nchini humo wakiwa wamejikusanyia alama 23 msimu huu huku wakiwa wamecheza michezo 17.

Bado hawajatoa taarifa rasmi ya ujio wa msafara wao, japo watapaswa kufika mapema kabla ya wikiendi kuzoea mazingira ya jiji la Dar es Salaam.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic