April 2, 2018



Wakati wapinzani wa Yanga wakitarajiwa kuwasili nchini wiki hii, Wanajangwani hao tayari walishapata mbinu za Waethiopia hao Uwanjani.

Yanga wataingia wikiendi hii Uwanja wa Taifa kukipiga na Welayta Dicha katika mchezo wa Kombe la Shirikisho huku wakiwa tayari washawasoma aina ya mchezo wanaoutumia Uwanjani.

Wakati Yanga ikielekea Morogoro kuweka kambi ya muda mfupi kujiandaa na mechi ya Kombe la FA dhidi ya Singida United, Kocha George Lwandamina alikuwa amesafiri kuelekea Ethiopia.

Taarifa zilieleza kuwa Lwandamina alienda kuwasoma wapinzani wao Welayta Dicha ili kujua mbinu zipi huwa wanazitumia Uwanjani kabla hawajavaana nao kwenye mechi.

Safari hiyo ya Lwandamina nchini humo inaweza kuwa ina manufaa kwa Yanga kwa maana watakuwa wanajipanga kufanyia kazi madhaifu ya Waethiopia hao kabla ya kukutana nao Aprili 7 2018.

Kwa namna ilivyo, Yanga watakuwa wamejitengenezea mazingira mazuri kuelekea mchezo huo wa Jumamosi ambao Yanga wanatakiwa kutumia faida ya Uwanja wa nyumbani kwa kufunga mabao mengi.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic