May 16, 2018


Pep Guardiola ameshinda tuzo ya Kocha Bora wa Ligi Kuu England kufuatia kuiwezesha Manchester City kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu nchini humo.

Guardiola ameisaidia City kufikisha pointi 100 msimu huu pamoja na kushinda jumla ya mechi 32 huku akipoteza michezo miwili pekee.

Mbali na ushindi huo, kikosi chake kimeweza kufunga jumla ya mabao 106 na kikiweza kwenda sare katika michezo minne.

Guardiola alijiunga na Manchester City msimu wa 2016/17 akitokea Bayern Munich inayoshiriki ligi ya Bundesliga.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic