May 16, 2018


Nahodha wa kikosi cha Yanga, Nadir Haroub 'Cannavaro', amewaomba mashabiki na wanachama wa Yanga kujitokeza kwa wingi Uwanjani wa leo watakapoikabili Rayon Sports ya Rwanda katika mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika.

Cannavaro amewahitaji mashabiki ili kutoa morali kwa wachezaji akiamini shabiki ni mchezaji pekee namaba 12 anayetoa mchango mkubwa pale anapojitokeza Uwanjani.

Mbali na hamasa, Cannavaro amewaomba mashabiki waje kwa wingi ili waweze kuipatia mapato Yanga ambayo imekuwa katika mwenendo usio mzuri kiuchumi hivi sasa.

Kikosi hicho kinataremka Uwanja wa taifa kuanzia majira ya saa moja jioni kucheza mtanange huo wa pili katika hatua ya makundi ya michuano hiyo.

Salehjembe.blogspot.com inawatakia kila la kheri Yanga kuelekea mechi hiyo ya kimataifa.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV