June 2, 2018


Wakati ikiwa imesalia siku moja kuanza kurindima kwa michuano ya SportPesa Super Cup nchini Kenya, miamba wa soka nchini Tanzania, Simba na Yanga wamegoma kulala Hotel Moja mjini Nakuru, Kenya.

Imeelezwa kuwa baada ya kuwasili nchini humo timu hizo mbili zilipangiwa kuweka kambi kwenye Hotel ya Midlands iliyopo mjini Nakuru lakini ziligoma kuwa pamoja eneo hilo.

Msala huo ulitokea mpaka ambapo ikabidi watenganishe na Yanga walisalia kwenye Hotel hiyo huku Simba ikabidi wapelekwe sehemu nyinginr tofauti na hiyo ambayo watani zao wa jadi waliamua kusalia.

Michuano hiyo inayoanza kesho Jumapili, itaanza kwa Yanga kukipiga na Kakamega Home Boys kuanzia majira ya saa 7 kamili mchana huku JKU ya Zanzibar ikicheza na Gor Mahia FC saa 9 mchana.

Wakati huo Simba yenyewe itaanza kibarua chake Jumatatu ya wiki ijayo Juni 4 2018 kwa kukipiga na Kariobang Charks kuanzia majira ya saa 9 kamili mchana.

1 COMMENTS:

  1. Waandaaji hawako makini. Unawezaji kuziweka timu pinzani kwenye hoteli moja ? Sababu yake nini kama si kukaribisha uwezekano wa kuhitilafiana na kukzua kutoelewana? Kwanini viongozi hawatumii hekima? Ninawapongeza viongozi wa Klabu hizi waliogomea jimbo hili. Hatupendi kusikia wachezaji wa Simba na Yanga wametukanana nchini Kenya hotelini . Busara itawale kwa viongozi jamani hata hamuoni watu wa Sportpesa?

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic