June 2, 2018



Kikosi cha timu ya taifa ya Ufaransa kimeibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Italy katika mchezo wa kirafiki uliopigwa usiku wa leo.

Kipigo hicho cha Ufaransa kwa Italy ni mwendelezo wa ushindi baada ya kutoka kupata matokeo katika mchezo uliopita dhidi ya Ireland wa mabao 2-0.

Mabao ya Ufaransa yametikiwa kimiani na Antoine Griezmann kwa njia ya penati, Ousmane Dembele na Umtiti.

Mechi imekuwa kipimo kuelekea michuano ya Kombe la Dunia kwa Ufaransa inayotaraji kurindima siku chache zijazo nchini Urusi.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic