July 9, 2018


Imeripotiwa kuwa kiungo mkabaji kutoka klabu ya Kiyovu SC inayoshiriki Ligi Kuu nchini Rwanda, Fabrice Kakule, amewasili nchini kuja kufanya mazungumzo na Simba.

Kakule ametua nchini kufikia mwafaka na mabosi wa klabu hiyo ili kukamilisha dili la usajili tayari kuongeza makali katika safu ya kiungo kuelekea msimu ujao wa ligi na mashindano ya kimataifa.

Taarifa za ndani kutoka Simba zinaeleza kuwa mchakato wa kumpata mchezaji huyo umefanywa na Kocha Msaidizi, Masoud Djuma, ambaye ametoa pendekezo la kikosi hicho kutafutiwa mchezaji anayecheza nafasi ya kiungo.

Ujio wa kiungo huyo na dili lake likifanikiwa kukamilika, atakuwa anaungana na wachezaji wengine kama James Kotei, Jonas Mkude ambao wanacheza katika nafasi hiyo.

Ukiachana na Kakule, Simba pia wanahusishwa kuchukua saini ya Francis Kahata ambaye anakipiga Gor Mahia FCya Kenya ambaye yupo hapa nchini akishiriki mashindano ya CECAFA Kagame Cup.




9 COMMENTS:

  1. Chonde chonde simba msije mkamtoa Gyan kwa mkopo kama tetesi tulizozisikia..huyo dogo anapandisha timu sana..kama watakuja viungo wengine basi msione aibu kumtoa niyonzima ama kotei ama wote kwa mkopo..waingie wengine wanaofiti zaidi.. kotei anacheza vizuri nyuma zaidi kuliko akicheza kiungo lakini bado pia anamakosa mengi akicheza kama beki.

    ReplyDelete
  2. Mbona wachezaji wa kigeni watakuwa 9 sasa wakati mwisho ni 7

    ReplyDelete
    Replies
    1. Labda TFF wamebadili utashangaa wakasema mwisho kumi kwa vile ni simba

      Delete
  3. Timu INA viungo was kutosha, sioni sababu ya kuongeza viungo. Nionavyo mahitaji ni wings hasa upande was Julia na beki 1 wa kulia kusaidia. Nurdin Chona kwa mfano anastahiri ili kuziba pengo la Kapombe iwapo ni majeruhi au mgonjwa au iwapo kapangwa nafasi zinginezo. Pia TFF iruhusu usajili was wachezaji 10 was kigeni sioni ka kuna tatizo. Wanaweza kuweka utaratibu tu kuwa wanaohitajika kucheza uwanjani wasizidi 7, ndani ya wachezaji 11. Sio tatizo Tanzania inatakiwa kubadilika tusiwe waoga. Tuangalie wenzetu MF DRC bado wapo vzr pamoja na kuruhusu wachezaji wa kigeni hats timu nzima.

    ReplyDelete
  4. Simba sasa hivi inamwitaji Kahata tu, wengine wasubiri

    ReplyDelete
  5. Hao wanaouliza eti wachezaji wa kigeni wapo tisa kwani usajili umeshafungwa?Kuna mchujo utakaotokea kwa wachezaji wote wa kigeni na wapya.Baada ya hapo itajulikana nani kabaki .Nani kaachwa nä yupi katolewa kwa mkono.Sasa hivi kuhukumu ni mapema min.Kuweni nä subira.

    ReplyDelete
  6. Nimeshamstukia kocha Masoud Djuma.Ataivuruga timu.Mie naona kina Kazimoto, Ndemla, Muzamir bado viungo fresh tu labda huyo kiungo Francis Kahata au vunja bank nunua Tshimbi

    ReplyDelete
  7. Wachezaji wa kimataifa wa kiwango cha hali ya juu na wenye uzoefu wanahitajika kuisaidia Simba katika mechi za kimataifa, ila ni msimamo wangu kuwa wachezaji kutoka nchi za Afrika Mashariki hawawezi kutusaidia katika mechi za kimataifa hawazidiani na wachezaji wa bongo

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic