July 9, 2018


Uongozi wa timu ya soka ya Gor Mahia ya Kenya, umeitaka Simba kutuliza mzuka katika harakati zake za kumwania kiungo wao mshambuliaji, Francis Kahata.

Simba inadaiwa kuwa katika harakati za kumwania mchezaji Kahata, baada ya kuvutiwa na uwezo wa juu aliouonyesha katika michuano ya SportPesa iliyofanyika nchini Kenya hivi karibuni na Gor Mahia kuibuka mabingwa wa michuano hiyo.

Habari za kuaminika kutoka ndani ya Simba ambazo Championi Jumatatu limezi­pata zimedai kuwa uongozi wa Gor Mahia umewaambia Simba kuwa utawapatia mche­zaji huyo mwezi Desemba kama kweli wanamtaka lakini siyo hivi sasa.

Sababu kubwa ya kufanya hivyo ni kwamba bado wa­naihitaji huduma yake kwa ajili ya michuano ya kimataifa ya Kombe la Shirikisho Afrika ambayo timu hiyo inashiriki na ipo kundi moja na Yanga.

“Juhudi zetu na kumsajili Ka­hata bado tunaendelea nazo lakini Gor Mahia wamekuwa wagumu sana kumwachia na wametuambia kuwa bado wa­nahitaji huduma yake katika michuano ya kimataifa.

“Wametuambia kuwa kama tunamtaka kweli basi wao watamwachia mwezi Desemba mwaka huu, lakini kwa sasa itakuwa ni ngumu,” kilisema chanzo hicho cha habari na kuongeza kuwa bado wanaende­lea kupambana ili kuona kama watafanikiwa kumpata kabla ya ligi kuanza.

Hata hivyo, baadhi wa vion­gozi wa Simba walipoulizwa kuhu­siana na suala hilo, hawakuwa tayari kusema chochote zaidi ya kudai kuwa anayeweza kulizun­gumzia hilo ni kaimu rais wa klabu hiyo, Salim Abdallah ‘Try Again’ ambaye ndiye amekuwa akisima­mia shughuli zote za usajili klabuni hapo lakini alipotafutwa simu yake ya mkononi iliita muda mrefu bila ya kupokelewa.

CHANZO: CHAMPIONI

3 COMMENTS:

  1. Simba fanyeni juu chini Kahata acheze na mkude pale kati patakuwa pa moto sana.

    ReplyDelete
  2. Achaneni naye hakuna haja ya kulazimisha wako viungo wengi wenye ubora wa hali ya juu kuliko huyo....ulizieni mascout wa Ghana, Senegal, Misri...under 23 years

    ReplyDelete

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV