November 20, 2018


Ofisa Habari wa klabu ya Simba ameibuka na kueleza namna ambavyo hajaeleweka kuhusiana na andika lake fupi la jana juu ya beki wa Simba, Shomari Kapombe.

Manara ameandika kuwa hakumaanisha TFF huwa hawahusiki kuwasaidia wachezaji pale wanapoumia katika timu ya taifa bali wao kama klabu wameamua kumuwahisha Kapombe kwa ajili ya matibabu.

"Niwasihi watu wetu tunaposoma vitu makini tusizushe hisia zetu . Jana niliandika kuhusu Beki wa nchi Shomari Kapombe kwenda kutibiwa nje na nikaeleza kwa kina! Kuna wasiotaka kuelewa eti TFF hawahudumii wachezaji.

"Narudia TFF na Simba siku zote kama inavyopaswa tupo pamoja, na katika hili mnielewe hivyo.

"Na naomba msamaha kwa TFF kwa kutoeleweka vema!
Sasa tayari Shomari ashaanza vipimo na tutawajuza zaidi" ameandika Manara.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic