November 20, 2018


Mshambuliaji wa timu ya Azam FC, Donald Ngoma ataukosa mchezo wa timu yake dhidi ya Ruvu Shooting kutokana na adhabu ya kadi nyekundu aliyoipata katika mchezo wa ligi kuu dhidi ya Kagera Sugar.

Ngoma mwenye mabao 3 mpaka sasa alipewa kadi hiyo baada ya kujibizana na mwamuzi wa mchezo huo hali iliyopelekea kupewa adhabu hiyo.

Kocha Msaidizi wa Azam FC, Iddy Cheche amesema kuwa wanatambua kuwa ataukosa mchezo huo ila hawana namna watanafikiria namna ya kumpata mbadala wake.

"Ni mchezaji mzuri ambaye tayari alishaanza kuelewana na wachezaji wenzake na ndio maana alikuwa akikosa bao basi anatengeneza pasi ya bao, hivyo tutampanga mchezaji mwingine atachukua nafasi yake," alisema.

Azam wamecheza michezo 12 bila kupoteza hata mchezo mmoja wakiwani vinara baada ya kujikusanyia pointi 30.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic