ETIENNE
Ndayiragije, Kocha Mkuu wa Azam FC amesema kuwa ndani ya kikosi chake kuna
tatizo kubwa la lugha kwa wachezaji wake kushindwa kuelewana jambo ambalo
linamfanya ashindwe kubadili safu yake ya ulinzi.
Mpaka sasa
safu ya ulinzi ya Azam FC ipo chini ya beki Nicholaus Wadada, Bruce Kangwa,
Yakub Mohamed na Daniel Amoah, huku mlinda mlango akiwa ni Razack Abarola ambao
aliwatumia kwenye mchezo wa kimataifa dhidi ya Fasil Kenema na aliwatumia pia
kwenye mchezo dhidi ya KMC wa Ligi Kuu Bara.
Kwenye
mchezo dhidi ya Fasil Kenema ambao ulikuwa wa marudiano wa Kombe la Shirikisho Afrika,
Azam FC ilishinda kwa mabao 3-1 na ule dhidi ya KMC ilishinda bao 1-0.
Akizungumza
na Saleh Jembe, Ndayiragije amesema kuwa sababu kubwa inayomfanya ashindwe
kubadilisha safu ya ulinzi ni Lugha ya Kiingereza ambayo wanaitumia.
“Mabeki
wangu wanaitumia lugha ya Kiingereza, nashindwa kuwabadilisha hawa kwa
kuwa nikiweka wachezaji wengine hakuna atakayeweza kuelewana na wengine, jambo
ambalo linanifanya niwatumie muda wote,” amesema Ndayiragije.
0 COMMENTS:
Post a Comment