JACKSON
Mayanja, Kocha Mkuu wa KCM amesema kuwa kinachowashinda wachezaji wake kwa sasa
kupata matokeo ni kushindwa kutumia akili wakiwa uwanjani na badala yake
wanatumia nguvu nyingi.
KMC ilianza
kufungua pazia la ligi kwa kuambulia kichapo cha bao 1-0 mbele ya Azam FC
mchezo uliochezwa uwanja wa Uhuru.
Akizungumza
na Saleh Jembe, Mayanja amesema kuwa kwa sasa mpira umebadilika hauhitaji kutumia
nguvu nyingi bali akili pamoja na mbinu uwanjani.
“Wachezaji
wangu wengi nimekuwa na kazi kubwa ya kuwafundisha namna ya kutumia akili na
sio nguvu ndicho ambacho kinatuponza kushindwa kuwa na matokeo chanya kwenye
mechi zetu za mashindano.
“Hilo
limechangia mimi kufungwa na Azam FC pia nina lundo la majeruhi ambao mpaka
sasa sijawatumia na ninalazimisha kuwatumia wachezaji ambao wanacheza nafasi
wasizozijua kwa asilimia mia,” amesema Mayanja.
0 COMMENTS:
Post a Comment