August 28, 2019


Aliyewahi kuwa mchezaji wa Yanga, Ally Mayay Tembele, amelitaka benchi la ufundi la timu hiyo chini ya Kocha Mkuu, Mwinyi Zahera, kuhakikisha inafanyia kazi mapungufu yaliyo katika safu ushambuliaji, kabla hawajakutana na Zesco United katika Ligi ya Mabingwa Afrika.

Mayay ameamua kufunguka akiamini kuwa Yanga bado ina mapungufu katika idara hiyo kutokana na namna walivyocheza kwenye mechi ya mkondo wa kwanza dhidi ya Township Rollers jijini Dar es Salaam.

Mayay ameeleza Yanga haikufanya vizuri walipocheza na Rollers jijini Dar es Salaam, akisema kwa namna wanavyocheza mbele wanaweza wakashindwa kupata matokeo mbele ya Zesco.

"Yanga bado ina mapungufu mengi katika idara ya ushambuliaj, na hilo limekuwa tatizo kwa timu nyingi hapa Tanzania.

"Ni vema Kocha akajaribu kulitazama tatizo hili kwa jicho la tatu ili kuongeza makali na umakini timu iweze kufanya vizuri, uwepo wa wachezaji kama Juma Balinya, Patrick Sibomana unahitaji muda kujenga muunganiko wa safu zuri maana bado ni wageni" amesema Mayay.

Aidha, kwa upande mwingine Mayay ameeleza katika nafasi ya ulinzi Yanga haina matatizo kama ilivyo mbele hivyo uwepo wa Yondani utaisaidia kuzuia makali ya Zesco kutokana na uzoefu wake.

"Uwepo wa Yondani katika idara ya ulinzi utaisaidia Yanga kudhitbiti mianya ya wapinzani, na hii ni kutokana na uzoefu mkubwa alionao katika michezo ya kimataifa.

"Yondani amekuwa akiwaongoza wenzake vizuri pindi wanapokuwa dimbani lakini pia hapaswi kuttegemewa peke yake zaidi ya kucheza kitimu."

Na George Mganga


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic