August 27, 2019


Azam FC imefanikiwa kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya KMC FC, mechi ikichezwa kunako Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.

Mechi hiyo iliyokuwa ya aina yake kwa timu zote mbili kucheza soka la kuvutia, ulimshuhudia mshambuliaji Idd Suleiman Nado akitupia kambani bao hilo katika dakika ya 15 ya mchezo.

Bao hilo limefanikiwa kudumu kwa dakika zote 90 mpaka mpira unamalizika matokeo yakiwa ni 1-0.

Timu hizo mbili zimekutana kwa mara ya kwanza katika ligi tangu kumalizika kwa msimu uliopita.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic