MWINYI Zahera,Kocha Mkuu wa Yanga amesema kuwa kikosi chake kipo sawa kuelekea mchezo wa marudiano dhidi ya Zesco utakapigwa kesho nchini Zambia.
Yanga inapeperusha bendera ya Taifa kimataifa na kesho itacheza mchezo wa marudio dhidi ya Zesco ikiwa na kumbukumbu ya kulazimisha sare ya kufungana bao 1-1 uwanja wa Taifa.
Zahera amesema kuwa: "Kupata sare mchezo wa kwanza haina maana kwamba hatuna nafasi ya kushinda uwepo upo na nia ya kufanya vema tunayo, ni wakati wetu kutumia makosa yetu kuyarekibisha na kutafuta matokeo.
"Kila mmoja anatambua namna michuano ya kimataifa ilivyo na ushindani nasi tunatambua kwamba tunakitu ambacho tunakitafuta kitapatikana, mashabiki watupe sapoti," amesema.







Subirini mchezo uchezwe jamani msijipe matumaini wakati hata mchezo haujachezwa mwishowe mtakuja kulia na kuumia....hili ni tatizo kubwa la timu matokeo ya soka wanakuwa nayo mdomoni na propaganda kibao halafu mwisho wa siku matokeo yanakuwa tofauti hapo ndipo unaposikia watu wamekufa wengine wako mahututi wengine wamezimia subirini dakika 90+ ziishe na matokeo yatajulikana....kwasasa hivi muwe wakimya kwani hamjui au hakuna mtu anayejua matokeo mpaka dk 90 za mchezo!
ReplyDeletekwa hiyo jamaa ulitaka kocha aseme anaenda kufungwa huko zambia?
Deletejamani sio kila jambo la kukosoa, ni nani anaekwenda kwenye mapambano akase.a mi naenda kuwakilisha tu asitegemee ushindi.
Kocha aseme tumejiandaa vilivyo kuhusu ushindi tusubiri baada ya filimbi ya mwisho dakika 90....hivyo ndiyo majibu ya hilo swali
Delete