BONDIA wa ngumi za kulipwa nchini, Issa Nampepeche anatarajia kupanda ulingoni dhidi ya Alli Hamis wa Morogoro katika pambano kuwapongeza mabondia walioshinda mikanda ya ubingwa kimataifa.
Katika pambano hilo linalofahamika kama usiku wa mabingwa likiwa chini ya udhamini wa gazeti la Championi na +255 Global radio linatarajia kufanyika Oktoba 4, mwaka huu kwenye Ukumbi wa Club 361 uliopo Mwenge, Dar.
Akizungumza na Championi Ijumaa, Mratibu pambano hilo, Selemani Semunyu alisema mipango imekamilika ikiwemo mabondia watakaocheza licha ya kupokea maombi mengi ya mabondia wanaotaka kushiriki kuonyesha furaha yao na kuwaunga mkono mabondia waliofanya vizuri kimataifa.
Semenyu amewataja mabondia watakaopongezwa siku hiyo ni Abdallah Pazi ‘Dullah Mbabe’, Tony Rashidi ,Bruno Vifua Viwili na Nassib Ramadhani kufuatia kuiletea sifa nchi kimataifa.
"Serikali na Wabunge wamewapongeza lakini wadau na mashabiki sasa huu ndio wasaa wa kuwapongeza hata kama kuna zawadi ya kuwapa hii ndio sehemu moja lakini tunawapongeza kwa pambano.
"Watakaofanya vizuri katika pambano hili wataweza kupata nafasi katika pambano la Desemba, mwaka huu katika pambano kubwa ambalo tumejipanga kulifanya.
Mapambano mengine siku hiyo yatakuwa ni Ibrahim Makubi dhidi ya Abdallah Kingolwira, Maganga Kulwa na Said Sudi, Hashimu Msungo vs Epson Lewis wakati Salumu Omari atamalizana na Ramadhani Chicho.







0 COMMENTS:
Post a Comment