December 24, 2019


MANCHESTER United ipo kwenye hatari ya kumpoteza nyota wao kinda Angel Gomes mwenye mpango wa kwenda ndani ya kikosi cha Barcelona.
Kinda huyo mwenye miaka 19 amesema kuwa ana mpango wa kuondoka ndani ya Old Trafford kwa ajili ya kutimiza malengo yake aliyojiwekea baada ya kushindwa kufikia makubaliano na mabosi wa United.
Gomez anakipiga pia kwenye timu ya taifa ya England ile ya chini ya miaka 20 alianza kulelewa ndani ya United akiwa na miaka sita amecheza jumla ya mechi saba za wakubwa na alianza tatu pekee za kwenye Ligi ya Europa. 
Habari zinaeleza kuwa mbali na Barcelona ambako anacheza mchezaji bora wa dunia, Lionel Messi pia Juventus na Craystal Palace zimeonyesha nia ya kuipata saini ya kinda huyo.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic