December 24, 2019


BONIFACE Mkwasa, Kaimu Kocha Mkuu wa Yanga leo ameambulia sare kwenye mchezo wake wa Ligi Kuu Bara akiwa ugenini mbele ya Mbeya City mchezo uliochezwa uwanja wa Sokoine.

Sare hiyo imeipunguzia kasi Yanga ambayo ilikuwa inawafukuzia wapinzani wao Simba taratibu ambao kwa sasa wamewaacha kwa jumla ya pointi saba wakiwa ila Yanga ina mchezo mmoja mkononi.

Yanga imecheza jumla ya mechi 9 na ina pointi 18 huku Simba ikiwa imecheza mechi 10 na ina pointi zake 25 kwa sasa.

Mchezo wa leo Desemba 24 ulikuwa na ushindani kwa timu zote mbili huku kila timu ikitengeneza nafasi kwa kushtukiza na kushindwa kuzitumia kutokana na umakini wa mabeki wa timu zote mbili.

Yanga ilianza kufanya mabadiliko kipindi cha pili ambapo ilimtoa Said Juma dakika ya 61 na nafasi yake ikachukuliwa na Mrisho Ngassa ambaye alifanya majaribio mawili ambayo hayakuazaa matunda.

 Kwa upande wa Mbeya City wao walifanya mabadiliko dakika ya 67 kwa kumtoa Majaliwa Shaban na nafasi yake ikachukuliwa na Seleman Shaban na dakika ya 79 alitoka Idd Gammba na nafasi yake ikachukuliwa na Kelvin John kabla ya Notikasa Masasi kutoka dakika ya 85 nafasi yake ikahukuliwa na Seleman Mangoma na mabadiliko hayo hayakuleta matunda.

Kadi mbili za njano zimetolewa kwenye mchezo wa leo ambapo zote zimekwenda kwa Yanga alianza Deus Kaseke kuonyeshwa kisha Jaffary Mohamed kuonyeshwa dakika  ya 90 kwa kumchezea rafu mlinda mlango wa Mbeya City.

5 COMMENTS:

  1. Kasi gani hiyo ya mabingwa wa jadi ambayo leo ndio imepunguwa?

    ReplyDelete
  2. Kuna aina fulani ya uandishi inapofikia simba na yanga

    ReplyDelete
  3. Kiguru ns kiwete wamegawana pointi.

    ReplyDelete
  4. Basi unaambiwa Mbeya ilikuwa na upunngufu wa nyota wake saba na huku wakiwa tayari wameshafugwa magoli 12

    ReplyDelete
  5. This comment has been removed by the author.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic