KOCHA Mkuu wa Yanga, Luc Eymael amesema kuwa Kagera Sugar wamewaotea kuwachapa mabao 3-0 hivyo leo watawasha moto mbele ya Azam FC Uwanja wa Taifa.
Eymael alianza kazi yake ya kwanza ndani ya Yanga kwa kichapo cha mabao 3-0 mbele ya Kagera Sugar leo ataongoza jahazi lake kwenye mchezo wa pili dhidi ya Azam FC.
"Haina maana kupoteza kwa kufungwa mabao 3-0 mbele ya Kagera Sugar timu yetu itaendelea kufungwa hapana, walitufunga kwa kuwa walituotea hawataweza kuendelea kutufunga tena tutapambana kufanyia kazi makosa yetu.
"Tatizo bado wachezaji hawajawa na muunganiko mzuri hasa kwenye umaliziaji hapo mambo yakikamilika kila kitu kitakwenda sawa, mashabiki waendelee kutupa sapoti," amesema.
Yanga imecheza jumla ya mechi 13 ipo nafasi ya nane ikiwa imejikusanyia pointi zake 25 leo itamenyana na Azam FC iliyo nafasi ya tatu na pointi 29.
Kwa Azamu ninavoiona mimi, Yanga isijipe tamaa kubwa kwa jinsi hali yake ilivo hivi sasa na bora waingie kimyakimya bila ya vishindo vya majigambo kwasababu majigambo yataifanya Azam wazidishe nguvu zaidi
ReplyDelete