UONGOZI wa Simba umesema kuwa watani zao wa jadi Yanga hawataweza kuvunja rekodi waliyoiweka wao kwenye kilele cha Simba day kuanzia perfomance mpaka mkwanja watakaoingiza kwa fedha za kiingilio.
Haji Manara, Ofisa Habari wa Simba amesema kuwa mipango yao ilikuwa tofauti na wamefanya mambo ambayo ni hatua nyingine kabisa kwenye uwanda wa michezo.
Simba jambo lao walilikamilisha Agosti 22 ambapo ilikuwa ni kilele cha Simba day na walimshusha msanii Diamond kwa Helkopta ndani ya Uwanja wa Mkapa.
Yanga wao jambo lao linafika kilele Agosti 30, Uwanja wa Mkapa nao pia wanamshusha Harmonize kwenye kilele cha Mwananchi jambo ambalo Simba wamesema kuwa hawawezi kufikia walipofika wao.
"Kuanzia kiingilio ilikuwa ni juu na tumeingiza pesa nyingi ambazo wao wengine watashindwa kuivunja. Ikiwa watavunja itakuwa ni maajabu kwa kuwa kiingilio chao wao kinaanzia buku tano sasa watawezaje kutufikia sisi?
"Ishu ya shoo, ujue kumshusha Diamond kwenye jukwaa sio kitu kidogo, Diamond n msanii mkubwa na anapendwa hivyo hebu tusubiri na tuone itakuaje na hiyo Mwananchi day lakini cha msingi ambacho ningewashauri kwanza wahakikishe anakuja kocha kwanza maana ligi inakaribia kuanza," amesema Manara.







Hamuwezi kufanana kwa kuwa hata kuzaliwa kwa klabu kulitofautiana,na majina pia tofauti.acha ushamba! Helkopta ndiyo nini? acheni ulimbukeni washamba nyie.
ReplyDeleteMo alipandisha kiingilio na kujitwisha kazi ya Manara ili apate fedha 20 Bilioni anayodaiwa na mikia ili anunue timu jumla na haondokane na aibu ya kudaiwa. Kama ni uongo Manara awaeleze leo Wana Mikia fedha hizo zimewekwa Akaunti gani?
Deletekuna wengine wanauliza helkopta nini hawalijui 😆😀😀
ReplyDeleteYanga wanasema wameishtakia Fifa kama kweli kuhusu Morrison kuwa mchezaji wao na majibu huweza Kuchukuwa miezi, Jee kabla ya majibu ikafika ile tarehe ya mchezo wa ligi baina Yanga na Simba na Morrison ndani, Yanga itacheza au itagomea?
ReplyDeleteUnakijua kibar Cha Kaz wew unaeuliza kuhusu Morrison!? Yangaaaaa wamezui kibar chake kw hyo hawez fanya Kaz sehem nyingine
ReplyDeleteKuhusu kibali cha kazi wizara husika itaangalia sheria inasemaje na ndiyo itakayowaongoza kufanya uamuzi wa Morrison wakati Yanga wakisubiri majibu ya FIFA
DeleteKuhusu kibali cha kazi kwa Morrison wizara husika itaongozwa na sheria kufanya maamuzi
DeleteSoma Bernard Morrison transfer utaona fifa imempeleka wapi ok
ReplyDelete