HUBERT Velud, raia wa Ufaransa inaelezwa kuwa yupo kwenye mazungumzo na baadhi ya mabosi wa Yanga wakiwa na mpango wa kumpa dili la kukinoa kikosi hicho ambacho kwa sasa kipo chini ya Kaimu Kocha, Juma Mwambusi.
Velud mwenye umri wa miaka 61 anatajwa kupewa chapuo na baadhi ya viongozi wa Yanga kwa kuwa anauzoefu na soka la Afrika.
Amewahi kuwa Kocha Mkuu wa TP Mazembe msimu wa 2016, Etoile Sportive du Sajel msimu wa 2017, pia USM Alger na ES Setif jambo linalowapa nguvu viongozi wa timu hiyo kumpa mkataba.
Raia huyo wa Ufaransa ambaye nafasi aliyokuwa anacheza ilikuwa ni kipa anapewa chapuo la kuwa mrithi wa Kaze.
Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Yanga, Mshindo Msolla amesema kuwa utaratibu wa kumpata mrithi wa Kaze unafanyika na hivi karibuni atatambulishwa kwa mashabiki.
"Kila kitu kuhusu kumpata mrithi wa Kaze kipo sawa na ipo kamati ambayo inashughulikia masuala ya upatikanaji wa kocha, huko CV zitatumwa na mchakato utafanyika kupitia kamati ya utendaji," .
Almuradi mmeleta Mfaransa nasi pia tualeta Mfaransa. Mnachokifanya nai twakifanya nasi pia tunayo hela Mpaka ijulikane
ReplyDeleteWe jamaa unatisha jana ulituwekea msebia leo mfaransa sijui kesho utaibuka na yupi
ReplyDeleteInawezekana akaja mfaransa maana simba walipoleta mbelgiji na wao wakaleta mbelgiji yanga akiwa na mserbia na simba hivyohivyo hivi vilabu ni full kuigana
ReplyDeleteYanga wanatakiwa kwanza kabisa wamtoe mwenyekiti.mwenyekiti anaigilia majukumu ya makocha. Kipind cha mwinyi zahera. Zahera alisema anaigiliwa panga kikos. Sasa jiulize mwenyekiti anaigilia majukumu ya Kocha Kama unaweza ww mwenyekiti Kocha mlimuajili wann.msolla ndo kilus cha yanga. Hasitahili kuwa mwenyekiti huyo.nibola wagemchaguaga jonas thiboloa
ReplyDelete