July 31, 2021

INAELEZWA kuwa klabu ya soka ya Simba ipo kwenye mipango ya kumsajili kiungo mkabaji wa klabu ya Kagera Sugar, Abdulswamad Kassim ‘Guty’ ili kukiongezea nguvu kikosi hicho kuelekea msimu ujao. 

Simba inataka kuongeza ufanisi wa nafasi hiyo ya kiungo mkabaji, hasa baada ya kuwepo kwa sintofahamu ya utovu wa nidhamu wa mara kwa mara wa Jonas Mkude.

Nafasi ya kiungo mkabaji ndani ya Simba kwa sasa ina wachezaji wawili wa asili ambao ni Mzamiru Yassin, na Mganda, Taddeo Lwanga.

13 COMMENTS:

  1. ĢUTY, unaenda kuua kipaji chako huko, achana nao hao, pesa utakazo pokea ndio zitakazo kupoteza katika maisha ya soka, kama Yanga au Azam wanakuhitaji nenda huko angalau utapata nafasi ya kucheza, Simba inaua vipaji vya wachezaji wazawa , achana nao.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Kama imekuuma chomoa!! Simba ina ua vipaji, wako wapi kina Gadiel Michael, Ibrahim Ajibu, Charles Illafya, Ibrahim Ame, Said Ndemla, na wengineo wengi tu.... Simba inaua vipaji, wachezaji wazawa timu za kusajili ni Azam au Yanga tu, huko utalinda kipaji chako na marupurupu ni mazuri, Simba ina ua vipaji vya wachezaji wazawa, timu ina endeshwa kihunihuni, kiujanja ujanja. Ikataeni hiyo timu.

      Delete
    2. Kupanga ni kuchagua; ubaki na kipaji bila pesa, au upate pesa kipaji kipotee. Tuna wachezaji wa zamani ambao wamebaki na sifa za kijinga tu kwamba walikuwa wakali, lakini maisha yao ni ya kutia maji tia maji

      Delete
    3. kwa hiyoo wee Dokta unaamaanisha Yanga na Azam ndo kuna wachezaji wasio na uwezo kwamba huyu mchezaji akifika tuu anaingia kikosi cha kwanza na anacheza au

      Delete
    4. Yuko wapi paul godfrey boxer,yupo wapi makapo yupo wapi waziri yupo wapi kabwili

      Delete
    5. Simba ndo inaua vipaji et, mawazo ya hivyo et Simba inaua vipaji, unataka mchezaji afike kukimbiakimbia na apangwe tu kisa ni mzawa. Wazawa mbona wapo wengi Simba wanaofanya vizuri. Kapombe, mzamiru, Boko, husen, mkude,maisha ni kupambana. Ni wangapi walifika yanga wakiwa wzuri lakini mwisho wa siku wanaondoka yanga wakiwa katika viwango vya hovyo. Acheni mawazo ya utaputapu hayo

      Delete
  2. Mwanaume kajengwa na Mungu kwaajili ya kupambana ila sisi watanzania akili zetu zimejikita katika uvivu na uoga.Hakuna kipya Cha ajabu anachokifanya Miqisone kijana wa kitanzania ashindwe kufanya ni kujitambua na kujituma tu.

    ReplyDelete
  3. Simba wala hawamjui huyo mchezaji!ni akili za mwandishi kumpa promo tu,labda aende Coastal Union au Ihefu

    ReplyDelete
  4. Saleh Jembe mtapoteza heshima yenu. Post zenu nyingi za utafiti (zisizo habari za matukio) ni uongo! Badilikeni vinginevyo mtaonekana medium ya Udaku!

    ReplyDelete
  5. Wachezaj wakibongo wavivu tu,mbona akina boko ,mzamiru,kapombe fresh tu.

    ReplyDelete
  6. Iyo Azam Ndio bingwa wa kuua vipaj

    ReplyDelete
  7. Pana Bingwa wa Utapeli ilimradi usanihi,mpaka mnapewa hundi feki

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic