WAKATI yakisubiriwa kwa hamu maamuzi ya Mahakama ya kimataifa ya Usuluhishi wa Michezo (CAS), kuhusiana na kesi ya Yanga dhidi ya kiungo mshambuliaji wa Simba, Bernard Morrison kila upande umeonekana kuwa na matumaini makubwa ya kushinda huku tambo zikiendelea kutembea.
Kesi hiyo yenye usajili wa CAS 2020/A/7397 ilisikilizwa juzi Alhamisi Juni 29, mwaka huu ambapo baada ya kusikiliza mashauri ya pande zote mbili, mahakama hiyo iliweka wazi kuwa majibu ya kesi hiyo yatatolewa katika kipindi ya kati ya kesho Agosti mosi, mpaka Agosti 24, mwaka huu.
Katika kesi hiyo Uongozi wa klabu ya soka ya Yanga unadai uliingia na makubaliano ya mkataba wa miaka miwili na mchezaji huyo, huku Morrison yeye akidai kuwa mkataba wake halali ulikuwa wa miezi sita pekee.
Akizungumzia ishu hiyo Ofisa habari wa klabu ya Yanga, Hassan Bumbuli amesema: “Tunamshukuru Mungu kesi imeenda vizuri na baada ya taratibu zote za mashauri ya kesi kufanyika, sasa hivi utaratibu wa kawaida wa kufanya tathimini ya ushahidi uliotolewa hivyo watatoa maamuzi kati ya Agosti mosi, mpaka 24 mwaka huu.
“Ni kweli hatuwezi kuzungumzia hatima ya kesi hii, lakini tuna matumaini makubwa haki itatendeka hivyo Wanayanga wanapaswa kuwa watulivu wakati huu mahakama ikiwa inafanya maamuzi yake.”
Katika kilichoonekana kuwa ni
kijembe kwa Yanga, Morrison naye kupitia mtandao wa Instagrama ameandika: “Hata
katika wingi wa maji, bado mjinga ataendelea kuhisi kiu.”
Achaa anyooshwe, alitaka aombewe.
ReplyDeleteUtopolo Bado akili zao fupi
ReplyDeletewewe ndio akili zako fupi,yanga wanatafuta haki haki yao bwege mkubwa we
DeleteWanangojea ubingwa wanyanganywe Simba wapewe wao na Morrison kwa nguvu arejeshwe kwao kweli ni akili hiyo au ndoto ya bangi?
ReplyDeletehuna akili wewe mahakama ziliwekwa za kazi gani acha yanga watafute haki na mtanyooshwa tu
DeleteWatanyoka utopolo wanashida kweli bumbuli ajipange kufatwa na takukulu
ReplyDeleteHahahahhhhhh et hata kwenye wingi wa maji mjinga bado atahisi kiu
ReplyDeleteatahisi kiu yeye mwehu anayevua bukta uwanjani
DeleteYang waache kupoteza mda. Mbn wachezaj WAP weng .ten wazur zaid at ya b3
ReplyDeletesio kupoteza muda vicha kama akina morrison lazima tuwanyooshe
DeleteHaishi kutapatapa, atulie asubiri hukumu
ReplyDeletekama anajifanya mwendawazimu mwaka huu yanga itamtibu na mikia watamuona shubiri
ReplyDeleteHata hivyo Morrison alitoa hiyo comment kabla kesi haijasikilizwa....ilikuwa kabla ya kesi
ReplyDelete