July 12, 2021


 TAMBO zimezidi kutawala kuelekea kwenye mchezo wa Waliooa v Wasiooa unaotarajiwa kuchezwa Julai 30 huku kila timu ikitamba kwamba ‘litakufa jitu’.

Tayari kila timu zimeanza kujiweka sawa na wakiwasha moto wa maandalizi kwa timu zote mbili kwa wafanyakazi hao wa Global Group ambao huwa hawana jambo dogo.


Rekodi zipo wazi kwamba mchezo uliopita ubao wa Uwanja wa Sinza ulisoma Waliooa 2-1 Wasiooa hali hiyo ilifanya Wasiooa kuyeyusha furaha yao kwa kukosa ushindi kwa muda wa mwezi mzima.


Kwa Wasiooa ukiwaweka kando Smart Gin na Creative Bee ambao watatoa jezi pia wapo Peak Time Media, Tukuyu Spring Water, Global TV na +255 Global Radio wameweka mkono wao wa nguvu huku kwa wale Waliooa wakipigwa tafu na Saleh Jembe.

 

Ofisa Habari wa Wasiooa, Hussein Msoleka alisema kuwa kuna jambo kubwa litatokea kwa mashabiki wao kwa kuwa watashuhudia pira matata na mabao ya kuhesabu.


 Wibert Moland, mchezaji tegemeo kwa Waliooa alisema kuwa watapiga mpira wa kitabu na kuwapa kichapo cha maana wapinzani wao.

 

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic