July 12, 2021


 UONGOZI wa Yanga umeweka wazi kwamba kuelekea kwenye mchezo wao wa Kombe la Shirikisho dhidi ya Simba, wataipiga kwenye mshono ambao waliwashona walipokutana Uwanja wa Mkapa.

Ikumbukwe kwamba Julai 3, Uwanja wa Mkapa ubao ulisoma Simba 0-1 Yanga ulikuwa ni mchezo wa  ligi na mtupiaji alikuwa ni Zawad Mauya.

Wanakwenda kukutana kwenye mchezo wa Kombe la Shirikisho, Uwanja wa Lake Tanganyika ikiwa ni mchezo wa fainali, Julai 25.

Akizungumza na Championi Jumatatu, Ofisa Uhamasishaji wa Yanga, Antonio Nugaz alisema kuwa wanakwenda kuwapiga wapinzani wao palepale kwenye mshono.

“Tulikutana nao Uwanja wa Mkapa bila wachezaji wenye majina tukaamua mchezo kupitia Mauya, sasa tunakwenda kuwapiga palepale kwenye mshono.

“Hamna namna sisi hatusemi sana ila tunatenda, tunajivunia mashabiki wetu ambao wapo pamoja nasi kila wakati, wadhamini wetu GSM pamoja na kazi kubwa ambayo inafanywa na Waandishi wa Habari kufikisha taarifa basi tukutane Kigoma,” alisema Nugaz.

 


11 COMMENTS:

  1. Mnyama katika mechi ile alikosea katika kipindi cha kwanza, lakini mambo yakabadilika kuanzia kipindi cha pili baada ya marekebisho na ilikuwa nusura nusura kubwa kwa Matopolo na huku penelti zikisepeshwa na hiyo tarehe 25 ndio boli litapoanza na ndipo porojo litapomalizika

    ReplyDelete
  2. Tukutane Julai 25 mtu anapigwa 4G

    ReplyDelete
  3. Mkavunje tena mageti

    ReplyDelete
  4. Kazi kubwa inayofanywa na waandishi wa havari ni ipi hasa, ya kueneza propoganda chafu dhidi ya mnyama? Kumbe ndio maana.....

    ReplyDelete
  5. Mikia safara hii wataenda kwa heshima na adabu, July 3 walijua easy game,wakaangukia pua.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Ushawahi kuona game yakubahatisha ina magoli zaidi ya moja?hata game ijayo ikiwa na goli moja ujue ni bahati.

      Delete
    2. Hakuna cha heshima Wala nn, Kikubwa waamuzi wawe makini muone kitakachotokea

      Delete
  6. Hivi kati ya yanga na simba nani anaongea sana?yanga mnapiga sana kelele yani sijui kwanini,mnaongea mpaka mnavuka mipaka,tuwaombeni jambo mngepunguza porojo maana zinaweza zikawatokea puani.

    ReplyDelete
  7. Hapo juu 6 kati ya 8 ni mikia, sasa nani mwenye kelele nyingi?

    ReplyDelete
    Replies
    1. Karibu kidimbwini kwenye utalii wa churaaaa wanaozaa teh teh teh

      Delete
    2. Huko sawa,hapa tunaongelea vichwa vya magazeti na blog,zinaongoza kwa habari za yanga sijajua kwanini?ingawa utapinga ila huo ndio ukweli

      Delete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic