MWANA FA |
Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal Malinzi, mapema wiki hii alijikuta
akijibizana hoja na mwanamuziki wa Bongo Fleva, Hamis Mwinjuma ‘Mwana FA’ juu
ya mwelekeo wa timu ya taifa, Taifa Stars, mara baada ya matokeo ya mabao 2-2
dhidi ya Msumbiji kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar, Jumapili iliyopita.
Mwana
FA ambaye ni mdau mkubwa wa soka, alitoa hoja kwa Malinzi katika mtandao wa
Twitter, ambapo alilalamika juu ya mahudhurio hafifu ya mashabiki katika mechi,
ambapo ilielezwa yalitokana na ukubwa wa kiingilio kilichopangwa na TFF, lakini
Malinzi alipinga hoja hiyo.
Sehemu
ya majibizano yao ilikuwa hivi:
Mwana
FA: Mheshimiwa Jamal Malinzi, nadhani hii kauli inatufaa na sisi...mahudhurio
hafifu yanashusha morali za wachezaji wetu.
Malinzi:
Mwana FA timu yoyote isiposhinda visingizio huwa havikosekani, Tanzania vs
Zimbabwe waliingia watu 8,000 tu na tukashinda, juzi waliingia 20,000 tukapata
sare.
Mwana
FA: Jamal Malinzi siyo lazima kushinda kila siku, kama mwanamichezo naelewa, ni
kuhusu kutengeneza mazingira 'yanayowabeba' wapenzi na wachezaji wetu.
Baada
ya hapo, Malinzi hakutaka tena kuendelea na mjadala huo licha ya wadau wengine
kuendelea kutoa maoni mtandaoni hapo, ambapo wengi wao walionekana kuitupia
lawama TFF kutokana na kuweka kiingilio cha chini kuwa shilingi 7,000 ambacho
walikilalamikia kuwa ni kikubwa.
0 COMMENTS:
Post a Comment