ALI KIBA AKIMTOKA CLAUD.... |
Bao la shuti kali la mita 24 alilolipiga kiungo mshambuliaji wa Yanga,
Geofrey Mwashiuya, lilimshawishi msanii wa Bongo Fleva, Ali Kiba kunyanyuka
kwenye kiti na kushangilia.
Mwashiuya alifunga bao hilo wakati timu yake ilipovaana na Telecom ya
Djibouti katika Kombe la Kagame, juzi Jumatano kwenye Uwanja wa Taifa jijini
Dar ambapo Yanga ilishinda 3-0.
Kiba alifika uwanjani hapo dakika tano baada ya mechi hiyo kuanza
akiwa amevaa jezi yenye rangi ya kijani na njano namba 8 yenye jina la kiungo
wa Yanga, Haruna Niyonzima.
Akiwa na marafiki zake, Kiba alionekana kuwa makini kufuatilia mchezo
huo huku kamera za SuperSport zikimfuatilia kwa makini.
Kiba alionekana kufurahishwa zaidi na mabao ya Malimi Busungu lakini
zaidi ni lile la Mwashiuya ambapo alishangilia kwa kuruka na kupiga makofi.
0 COMMENTS:
Post a Comment