August 23, 2015


Thierry Henry alikuwa gwiji la Arsenal, Walcott wakati akiwa mwokota mipira wa Southampton, alitamani siku moja angalau kupiga naye picha.


Alifanikiwa kufanya hivyo, siku alipojiunga na Arsenal. Alitamani kuwa kama yeye, Henry alipoondoka, alikabidhiwa jezi yake namba 14.

Woga ulimtawala akafikia kuomba namba 8, akaambiwa Samir Nasri anakwenda kujiunga na Arsenal tayari kapewa jezi hiyo, baadaye akakubali kuivaa namba 14.

Kumbuka, Walcott aliweza kuvuka, badala ya kupiga tu picha na Henry, akacheza timu moja pamoja naye.

Lakini baadaye akawa mrithi wa jezi yake na Henry aliporejea Arsenal kwa mkopo, safari hii Walcott ndiye alikuwa na jezi namba 14 na wakacheza timu moja.

Jifunze kujiamini, kuwa na nia ya kutimiza ndoto yako lakini kujiamini kwenda mbali zaidi ya karibu unapotaka kufika.





0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic