August 29, 2014



Mwenyekiti wa Yanga, Yusuf Manji amesema Simba wamekurupuka katika suala la Emmanuel Okwi.
Manji ameiambia SALEHJEMBE kwamba Simba wamefanya haraka kumsajili mchezaji ambaye ana mkataba na Yanga.

“Okwi bado ni mchezaji wa Yanga, ana mkataba na Yanga lakini ana kesi na Yanga.
“Simba wamekiuka sheria za Fifa kwa kumsajili mchezaji ambaye ana mkataba. Sisi tumemfungulia Okwi mashitaka akiwa bado mchezaji wetu na mkataba wetu naye haujaisha.
“Sasa walishindwa hata kutuuliza kuliko kukurupuka hivi,” alihoji Manji.

“Leo nitazungumza na waandishi, unaweza ukanisikiliza na kupata ninachosema lakini nakuhakikishia Simba wamekurupuka na wamevunja sheria na kanuni za Fifa kumsajili mchezaji mwenye mkataba na mtu mwingine.
“Sikuona sababu ya wao kujiingiza matatizoni,” alisema Manji ambaye anazungumza na waandishi leo saa tano asubuhi kuhusiana na suala hilo la Okwi.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic