September 30, 2014


Mechi za Ligi ya Mabingwa Ulaya leo zilikuwa na raha yake. Sasa iko hatua ya makundi lakini ushindani uko juu, angalia matokeo ya mechi za leo.



Sporting 0-1 Chelsea:
Sporting Lisbon ikiwa nyumbani, imeshindwa kuonyesha cheche baada ya kulambwa bao 1-0 na wageni wake Chelsea.
Licha ya juhudi za Luis Nani kutaka kuonyesha mchango wake tokea arejee Ureno, kikosi cha Jose Mourinho kilikuwa imara na Nemanja Matic ndiye alikuwa shujaa.

PSG 3-2 Barcelona:
PSG ikiwa nyumbani imefanikiwa kuifunga Barcelona kwa mabao 3-2.
PSG licha ya kucheza bila nahodha wake Zlatan Ibrahimovic ilionyesha soka safi na kufunga mabao matatu kupitia beki David Luiz, Marco Verrati na kiugo mtundu Blaise Matuidi lakini nyota Lionel Messi na Neymar nao wakajitutumua kufunga hayo mawili.

Man City 1-1 AS Roma
Vijana wa Manuel Pellegrini licha ya kuwa nyumbani, waliushindwa mziki wa AS Roma na kujikuta wakilazimishwa sare ya bao 1-1.
Man City walicheza vizuri na kupoteza nafasi nyingi na bao lao moja la Kun Aguero kwa mkwaju wa penalti halikuwasaidia hasa baada ya nahodha wa AS Roma, Francesco Totti kusawazisha.

CSKA Moscow 0-1 Bayern Munich:
Bayern Munich wamezidi kujiongezea pointi baada ya kufikisha sita kutokana na ushindi wa ugenini nchini Urusi.
Bao pekee la Muller, limewapa ushindi kama ule dhidi ya Man City katika mechi iliyopita.

MATOKEO MENGINE:
APOEL NICOSIA 1-1 AJAX 
SCHALKE 1-1 MARIBOR 
BATE 2-1 BILBAO
SHAKTAR 2-2 PORTO

MAPICHA ZAIDI YA ACTION, BAADAYE KIDOGO

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic