August 22, 2021


BEKI wa kati wa Yanga, Yanick Bangala Litombo amesema kuwa anasubiri kwa hamu kuanza kuitumikia klabu yake mpya ya Yanga tayari kwa msimu ujao katika mashindano mbalimbali ambayo timu hiyo itashiriki.

Litombo hivi karibuni aliachana na klabu ya Far Rabat ya nchini Morocco inayonolewa na kocha wa zamani wa Simba, Sven Vandenbroeck kwa kuvunja mkataba na klabu hiyo ili kukamilisha dili lake la kujiunga na Yanga kwa ajili ya msimu ujao.

Akizungumzia shauku yake Litombo amesema: “Nasubiri kuanza kufanya kazi ndani ya Yanga, kama ambavyo unafahamu kila kitu tumemalizana na Yanga na kilichobaki kwa sasa ni kutambulishwa tu na kuanza kazi rasmi kuitumikia klabu yangu hii mpya.

“Kila kitu kuhusu mipango na malengo ya timu nayafahamu, hivyo na mimi nipo pamoja katika kuhakikisha tunayatizimiza malengo hayo kwa pamoja kwa kushirikiana."

 


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic