November 21, 2014


Mhariri Kiongozi wa magazeti ya Championi, Saleh Ally, akifuatiwa na mwandishi wa magazeti hayo, Wilbert Molandi, wakitoa heshima za mwisho.

Mkurugenzi Mtendaji wa Global Publishers, Eric Shigongo, akitoa heshima.Mhariri Mtendaji wa magazeti ya Global Publishers, Richard Manyota, akipiga ishara ya msalaba kumuombea marehemu afike salama kwenye safari yake ya mbinguni.
Mwili wa marehemu Munyuku.
Mhariri wa michezo wa gazeti la Mtanzania, Mwani Nyangasa (kushoto) akitoa heshima za mwisho.
Mkurugenzi wa Redio One, Deogratius Rweyunga (kushoto) akitoa heshima za mwisho.
Michael Mukunza kutoka kampuni ya habari na mahusiano ya Executive Solution (kushoto) akitoa heshima za mwisho.
Mkuu wa Kitengo  cha Michezo wa New Habari House, Dominic Isiji (kushoto) akitoa heshima za mwisho.
Hapa safari ya kuupeleka mwili mkoani Morogoro kwa mazishi ilianza.
Mwili ukiwa ubebebwa na wanahabari.
Muombolezaji akiwa na msalaba wa marehemu Munyuku.
Mkurugenzi wa Global Publishers, Eric Shigongo (kushoto) akimfariji Mhariri Mtendaji wa magazeti ya New Habari House, Absalom Kibanda, kwa kifo cha mhariri wake.
Mhariri Kiongozi wa magazeti ya Championi, Saleh Ally, akimpa pole, mhariri wa gazeti la Bingwa.
Baadhi ya waombolezaji wakisikiliza utaratibu wa kuingia kwenye gari kwa waliohitaji kusafiri na mwili wa marehemu.
MWANDISHI mkongwe na mhariri wa magazeti ya New Habari House, Innocent Munyuku, aliyefariki usiku wa kuamkia juzi (Jumatano) akiwa usingizini, mwili wake umeagwa leo kwenye Hospitali Kuu ya Jeshi Lugalo Jijini Dar es Salaam na kupelekwa kwao Mazimbu mkoani Morogoro kwa ajili ya mazishi.
Katika maombolezo hayo ndugu, waombolezaji na wadau mbalimbali wa habari walijitokeza kumuaga mpendwa wao huyo.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic