December 18, 2014

Beki mpya wa Simba, Hassan Ramadhan 'Kessy' aliyejiunga na timu hiyo akitokea Mtibwa Sugar, anaonyesha ana mapenzi nayo tokea kitambo.

Katika picha zake zilizo kwenye ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Instagram, Kessy anaonekana akiwa amemkumbatia Simba wa sanamu kwa mapenzi makubwa.

Kessy amejiunga na Simba ambayo ilifanya juhudi na maarifa kumnasa, lakini Mtibwa Sugar ikaweka msimamo kutouza hata mchezaji mmoja.

Baadaye taarifa zilieleza kwamba Kessy ndiye aliushinikiza uongozi wa Mtibwa Sugar, kwamba anataka kuondoka na kwenda Msimbazi.

Kutokana na kuonyesha mapenzi makubwa, uongozi wa Simba ukaamua kumuachia, lakini ukaingiza chake.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic