September 3, 2015

Mshambuliaji nyota wa Tanzania, Mbwana Samatta amewaomba Watanzania kujitokeza kwa wingi Jumamosi kuinga mkono Taifa Stars.


Stars inashuka dimbani Jumamosi kuivaa Nigeria katika mechi ya kuwania kucheza Kombe la Mataifa Afrika.


Samatta amesema bado Tanzania ina nafasi licha ya ukubwa wa Nigeria lakini wnaawategemea Watanzania.

“Wao wanakuja kama wakubwa, huenda wakadharau wakijua wanapambana na Tanzania. Lakini nakuhakikishia tutapambana na kuhakikisha tunafanya vizuri.
“Hii ndiyo nafasi yetu, lakini Watanzania ni tegemeo letu kubwa na wamekuwa wakitupa nguvu kila wanapojitokeza na kutuunga mkono kwa nguvu.

“Ninawaomba wajitokeze kwa nguvu kutuunga mkono na sisi tutapambana na nguvu kubwa,” alisema Samatta.

Samatta, Thomas Ulimwengu wanaochezea TP Mazembe pamoja na Mrisho Ngassa anayekipiga Free State Stars ya Afrika Kusini wamejiunga na kambi ya Stars ambayo imewasili nchi baada ya kambi ya siku nane nchini Uturuki kujiandaa na mechi hiyo.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic