October 4, 2015


Mgombea wa Urais CCM, John Pombe Magufuli amemaliza kampeni zake mkoani Singida kwa kufanya mkutano mkubwa uliofanyika uwanja wa Peoples Singida Mjini. 

Katika mkutano huo walikuwezo wadau mbalimbali wa chama hicho akiwemo Mbunge wa zamani wa Singida Mjini Mohammed Dewji ambaye amekuwa mdhamini mkuu wa klabu ya Simba.

Katika Mkutano huo Mo aliwaaga rasmi wakazi hao na kuwaambia wamchague Mussa Sima wa CCM ambaye amemuachia jimbo hilo na kamwe wanasingida wasione kama amewatosa. Mo alisema ataendelea kuwasaidia endapo watamchagua Mbunge huyo wa CCM pamoja na madiwani wa Chama hicho.

Leo Magufuli ataanzia kampeni zake Kondoa mkoani Dodoma
.




0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic